Wednesday, August 20, 2014

Audio: Chidi Benz kufanya album ya pamoja na Fid Q

Siku moja baada ya kutambulisha wimbo mpya, Chidi ametangaza kuwepo kwa plan ya kuandaa album ya pamoja akiwa na Fareed kubanda "Rasheed vs Fareed"
Licha ya kuongelea album hiyo lakini pia amezungumzia ugumu wa mauzo ya album kwa wasanii na sababu zinazopelekea kuwepo kwa ugumu huo, kwa kuwa yeye alikuwa ni msanii wa hiphop aliewahi kuuza kopi nyigi wakati alipokuwa juu.

Video Teaser: Mi ni Star - Young Suma

Promising artist Young Suma ameachia teaser ya video ya wimbo wake "Mi ni Star
director ni chuck kutoka Mausay Records wakati beat  imetengenezwa na Levy wakati mixing na mastering imefanywa na Mike Kasanova kutoka future sound records
tazama hapa chini 

Video: Angalia interview ya Chidi Benz, Diamond na Dully ndani ya XXL

Jana kpitia XXL ya Clouds, Chidi Benz alitambulisha wimbo wake mpya "Mpaka Kuchee" akiwa amewashirikisha Diamond na AY huku beat ikiwa imetengenezwa na Dully 
Angalia video ya interview ilivyokuwa hapa chini 

Video: Anakonda - Nikki Minaj amchezea Lap Dance Drake

Nikki Minaj ameachia video yenye utata mkubwa baada ya kuonekana asilimia kubwa ya maungo yake wazi, huku akitingisha her behind kama wale dada zetu wa vigodoro
hakuishia hapo, Drake ameonekana katika video hiyo pia, akiwa amekaa kwenye kiti, huku nikiminaji akimkatikia kwa kumgeuzia mgongo.  Fanya kuitizama hapa chini

Tuesday, August 19, 2014

Picha: Kevin Harts amvisha pete mchumba wake wa miaka mitano

Mchekeshaji na muigizaji Kevin Hart amvisha pete mchumba wake "Eniko" katika siku yake ya kuzaliwa ambapo alikuwa akifikisha miaka 30.
Kevin alimpeleka dinner mchumba wake huyo na baadae kupiga goti mbele ya marafiki wengi waliokuwa nao pamoja, mmoja wa marafiki zake walipost video ya mwanzo wa tukio hilo na Eniko nae alipost mda mfupi baadae

Brand New Single: Chidi Benz feat Doiamond na AY, Na hiki ndicho kilimliza Chidi Benz leo akiwa studio za XXL

Baada ya kupotea kabisa kwenye game, Chidi Benz amerudi kwenye game na ngoma mpya akiwa na Diamond na AY
Ngoma inaitwa "Mpaka Kuchee" na beat imetengenezwa na Dully Sykes huku mixing kumaliziwa na Tuddi Thomas.
baada ya kuitambulisha ngoma hiyo leo kupitia xxl, chidi benz alilia sana kwa uchungu, machozi yakimtoka bila kikomo na baada ya kuulizwa sababu ya machozi yake hiki ndio alichokisema..

Sunday, August 17, 2014

Picha: wasanii walivyojiachia ndani ya fiesta 2014 Kahama Stadium

Picha: Wasanii wahojiwa ndani ya Kahama Fm

Baada ya wasanii kuwasili ndani ya wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga siku ya jana, leo hii wamepata nafasi ya kufanya mahojiano na redio ya Kahama inayoitwa Kahama Fm.
Baada tu ya kusalimiana na watangazaji wa Redio hiyo , Ally Tizee na Dj Rammi, watangazaji hao wakiwapisha Fetty na Bdozen na kuwaacha wakiendelea na interview hiyo ambayo walipiga story na wasanii wote wanaofanya show siku ya leo usiku..

Hivi ndivyo ilivyokuwa Fiesta ndani ya Bukoba

Sikuwahi kufikiria kama Bukoba ingeweza kuwa na watu wenye shangwe la hatari, ila ukweli ni kwamba, hata Mwanza ambapo Fiesta ndio imeanzia kwa mwaka huu, hawaifikii Bukoba kwa shagwe
Kila msanii aliepanda jukwaa hilo, alipigiwa shangwe mpaka akishuka unamuona ni mtu mwenye tabasamu la kutosha.
Nilikuwa nikiangalia show ikiendelea nikiwa backstage, hakika wasanii wote waliokuwa backstage wakiangalia msanii mwenzao akifanya yake jukwaani, mpaka wao walikuwa wakipiga shangwe kutokana na nyomi lililokuwa uwanjani lenye shangwe ailimia 100000

DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com