May 7, 2010

HII NDIO HISTORIA YA BONGO FLEVA


HISTORIA YA MUZIKI WA BONGO FLAVA

Historia ya muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava i hivi leo una historia ndefu kiasi kwamba hivi leo wengi hatukumbuki tena hata muziki huu ulianzaje,ukapitia hatua na harakati gani mpaka kufikia hapa ulipo hivi leo.
Miongoni mwa mashuhuda wa mwanzo wa harakati za mwanzo kabisa za muziki wa bongo flava ni aliyewahi kuwa DJ maarufu nchini Tanzania kwa jina Mike Pesambili Mhagama.Mike sio tu miongoni mwa mashuhuda wa mwanzo bali pia ni miongoni mwa watu wachache walioamini katika muziki wa kizazi kipya tokea mwanzo.Kumbuka hizo ni zile enzi ambapo muziki huo ulikuwa ukichukuliwa kama “uhuni” tu na sio aina mpya ya muziki au burudani.Ni watu wachache sana walioweza kutabiri hatua ambazo muziki huo ungepiga miaka kumi au kumi na tano baadaye.
Lakini pia Mike amekuwa akikerwa na jinsi ambavyo kumekuwepo na upotoshwaji au upindishwaji wa vipengele fulani fulani muhimu vya historia ya muziki huo. Katika kujaribu kuiweka vyema historia hiyo,Mike Mhagama ameandika kwa mapana na utulivu wa kina kuhusu harakati za mwanzo za muziki wa kizazi kipya,suluba walizopitia yeye na watangazaji wenzake katika kuutambulisha muziki huo,wadau mbalimbali anaowakumbuka katika harakati hizo,wanamuziki wenyewe,promoters wa muziki nk.
Pia Mike Mhagama,anaweka wazi kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakijiuliza;Nini chanzo cha neno Bongo Flava? Nani mwanzilishi wake?Kwa jibu hilo na historia nzima,kwa jinsi anavyoikumbuka Mhagama, msome kuanzia hapo chini,kwa maneno yake mwenyewe, kama tulivyoyanakili kutoka katika blog yake(kwa ruhusa na baraka maalumu).Habari imegawanyika katika sehemu nne ili iwe rahisi kwako kuzisoma na kuelewa vyema anachokizungumzia Mike Mhagama. Mwenyewe anasema yawezekana kabisa asiwe sahihi kwa asilimia zote na ndio maana anapenda kukaribisha hoja,maoni na masahihisho yoyote kutoka kwako msomaji.Mike Mhagama hivi sasa anaishi huko Los Angeles,California nchini Marekani.
CHIMBUKO LA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA NA MAANA HALISI YA NENO BONGO FLAVA.
Na Mike Mhagama-Los Angeles,Marekani.

1 comments:

  1. Daaamn hii photo imenikumbusha mbali sana,hasa mashindano yale ya yo rap bonanza new africa floor ya 11.muandaaji kim n the boyz.namuona hapo RAMSON,Y THANG,D ROB,EAZY B,NA MZEE WA RAP ZA KISWAHILI Jina limentoka.Msaada tutani pls tell me hao jamaa wako wapi????

    ReplyDelete


DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com