Nov 1, 2012

GARI LA JACKLYN WOLPER LACHOMWA MOTO

 

 
Jacqline ameandika kwenye blog yake na namkariri akisema “kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko salama”


U HEEEEARD: SAM MACHOZI ATIMULIWA NYUMBANI LOUNGE NA KUMWAGIWA MATUSI NA LADY JAY DEE


Mwanamziki Sam Machozi alie wahi kuwa katika bendi ya Machozi inayomilikiwa na Lady Jay Dee, atimuliwa katika mgahawa wa Nyumbani Lounge iliyoko Kinondoni  siku ya jumapili alipojisogeza eneo hilo kucheki mpira akiwa na wenzake, na hata baada ya kutoka nje alikutana na matusi kutoka kwa mwanadadiva Lady Jay Dee....aku mi simo wasikilize wenyewe hapo chini

UKIAMBIWA UNA AKILI ZA KITOTO KWELI UNA HAKI YA KUNUNA


 Huyu mtoto analazimisha kuingia kwenye gari, analia kwasababu hawezi kuingia, gari lenyewe ni Toy..inavyoonekana atakua wakishua, anawaona baba mama wanapanda yao, kwanini nae asipande yake hahahahhahaaaaa


CHRISS BREZZYYY ATUPIA SWAG ZA "KIOSAMA" KWENYE PARTY YA RIRI....KAMA ANASEMA "THIS TIME NO FIGHTS TUNAJILIPUA TU" LOOOOLSSS !!!

Breezy akiwa na washakji kama wanaenda kupachimba hivi......Next time atupie Mkwijuu sasa tuoneee..!
Ilikuwa Ni Halloween Party Ya Rihanna Huko Greyston Manor Ni Kati Ya Night Club Zinazobang Kwa sana Los Angeles.

BEN POL AINGIA KATIKA TASNIA YA BONGO MOVIE

Msanii wa Bongo Fleva wa kizazi kipya almaarufu kwa jina la Ben Pol anayetamba na ngoma kali hapa Tzee kama Nikikupata,Maumivu,Pete.
Latest info kutoka kwa msanii huyu ni kwamba baada ya kutoka na ngoma yake ya Pete sasa ameamua kuingia katika tasnia ya Bongo movie kwani alisema kwamba japokuwa zamani alishawahi kuwa Assistant Director katika movie ya Wrong number lakini leo hii anafunguka na kusema kwamba kwasasa ameshafanya movie mpya na karabani bila kusahau alimalizia kwa kusema kwamba mashabiki wake wakae tayari kwa ujio wake katika tasnia ya Bong movies.

Q CHIEF AFUNGUKA JUU YA SAKATA LA DIAMOND KUKOPI AIDEA YA NATAKA KULEWA KWA H BABA NDANI YA 255 NA MISS INFO

 Q chief atoa maoni yake juu ya sakata la Diamond kukopi aidea ya H baba, Dudu baya afunguka juu ya story ya kupigwa Geita asema hizo ni rumors zinazoletwa na watangazaji wawili ambao nina ugomvi nao na ugomvi huo ni kutokana na mimi kuwatetea na kuwapigania wasanii wa Mwanza haiwezekani miaka yote iwe ni Dudu Baya, Fid Q na H baba" zaidi msikilize hapa Miss InfoONE INCREDIBLE ANATARAJIA KUACHIA SOGA ZA MZAWA VOL II KITAANI

Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kwa jina la One Incredible anayetamba ngoma za kali kadhaa mpaka kupelekea mashabiki wa game la muziki wa hapa Tzee kumkubali zaidi katika kazi zake.
Latest info kutoka kwa msanii huyu ni kwamba jana baada ya kuongea naye aliniambia kwamba  anatarajia kuachia Soga za Mzawa vol 2.Kwa hiyo wale mashabiki wa HipHop wakae mkao wa kupokea ujio mpya wa One Incredible soon kuingia kitaani.

NU VIDEO: GELLY WA RHYMES "MEMORIES"


            

Z-ANTON SOON KUANDA VIDEO YAKE YA "SUPERSTAR"

 Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama Z-anto,ambaye anatamba na ngoma kadhaa hapa Tzee kama Mpenzi jini,Binti kiziwi,Kisiwa cha Malavidavi.
Latest info kutoka kwa msanii huyu ni kwamba baada ya kutoa ngoma yake ya Superstar sasa yuko njia kwa kufanya shooting ya video ya Super Star.Kwani alisema kwamba mara nyingi anapotoa ngoma zake katika vituo mbalimbali vya ma radio huwa kila baada ya wiki mbili ndiyo anaanza kuandaa mambo ya video.Baada ya kusema hivyo alimalizia kwa kusema kwamba pia anahitaji support kutoka kwako wewe mtanzania kwa ku push kazi wake.

JUST A PHOTO:MASANJA MKANDAMIZAJI AKIKANDAMIZA BREAK FAST YAKE

Mchekeshaji mahiri kutoka Original Komedi TBC1,Masanja Mkandamizaji leo asubuhi kupitia katika ukurasa wake wa Facebook aliamua kuweka picha hii ili aweze ku share na wewe Breakfast nzuri kama hii.Daaahh!!!! kweli mkandamizaji.

HAPPY BIRTHDAY AISHWARYA RAI BACHCHAN

Msanii mahiri wa Filamu za kihindi huko nchini indian,almaarufu kwa jina la Aishwarya Rai Bachchan leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 39 toka azaliwe mwaka 1973.Tunamtakia All the best katika game.

DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com