May 13, 2013

LINEX AMLIZA MAMA YAKE MZAZI MBELE YA UMATI WA MASHABIKI ZAKE


Msanii Linex ambae amejizolea mashabiki kibao kutokana na umahiri wake katika kutumia sauti yake, jana amemliza mama yake mzazai pale alipokuwa akifanya show yake ya bure mkoani alipozaliwa, Kasulu, Kigoma.
Tangu Linex alipoanza safari yake ya muziki takribani miaka 3, mama yake mzazi hajawahi kumuona na kumshuhudia mtoto wake live akifanya show.Ni katika uwanja wa ambapo mama alimshudia mtoto wake akiwa amejaza umati wa watu kuja kumshuhudia akifanya show, ndipo alipokutana na umati huo na jinsi kila mmoja alivyokua akimshangilia na kujikuta akimwaga machozi na kumsababisha Linex kuangua kilio pia akiwa mbele za mashabiki wake.
Linex aliamua kufanya show hiyo bure mjini kwao kwa ajili ya kutoa sapotio kwa wanao msapoti..

"yaani nimeshangaa sana kukuta umati wa watu uwanjani, unajua Kasulu ni mji mdogo sana so kukuta watu wote wale sijui hata wametoka wapi, ki ukweli mama yangu hajawahi kuniona nikifanya show, jana ndio ilikua mara yake ya kwanza, na alishangaa sana kuona watu ni wengi na wanashow love ya hatari..wakati mi naimba pale, nilimuona mama yangu na furaha mpaka anatoka machozi, ki ukweli nilijikuta na mimi naangua kilio tu, ila ilikua nzuri sana na watu wamefurahi sana" amesema Linex
18 comments:

 1. VoA ALITISHAA SANA HASA KWA KUKUMBUKA KWAO

  ReplyDelete
 2. Big up Linex keep it up bro much respect 4 what u dne,

  ReplyDelete
 3. big up bro keep it up, mch respect in what u did.

  ReplyDelete
 4. big up sana kwenu nikwenu tu, zawad kubwa sana iyo kwa mashabiki wako wa mkoa ulio zaliwa.

  ReplyDelete
 5. all the best in ur journey!

  ReplyDelete
 6. Umefanya vizuri sana Linex kwa kukumbuka home wewe ni wa maana sana tena kwa ndugu zako,mzoeshe mama kuona kazi zako ili ajue kuwa unakubalika na jamii,mpe hai.

  ReplyDelete
 7. salute kwake,its all bout showing love kwa hood member wake.

  ReplyDelete
 8. ninapo msikia linex nakumbuka
  day nilipokuwa kwenye send-off yangu saloon,
  naheshimu sana hii mutu.

  ReplyDelete
 9. UR THE BEST BRO.

  ReplyDelete
 10. Iko poa sana Linex

  ReplyDelete
 11. Cjaelewa hii nguo jamani mbona kama vikoti vya wadada vile vibajaji vinaitwa? Nikadhani mama kalia kwa sababu hii nilipoona kichwa cha habari mwanzo

  ReplyDelete
 12. still your ma no 1 artist brada!

  ReplyDelete
 13. Salute kwa Linex

  ReplyDelete
 14. hongera kwa kukumbuka kwenu

  ReplyDelete


DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com