Mar 1, 2013

H BABA: HAKUNA MSANII ALIEPIGA SHOW NYINGI KAMA MIMI 2012 NIMEPIGA SHOW 625

Msanii H baba leo hii amefunguka kupitia 255 ya xxl, kuwa hakuna msanii hata mmoja ambae ameweza kufanya show nyingi kama yeye kwa mwaka 2012, na kuwa, alifanya show 625 ndani ya mwaka huo..

"kama unajua mwakajana nimevunja rekodi ya show, hakuna msanii amepiga show nyingi kama mimi, mi nimepiga show 625, hakuna msanii kafikia rekodi yangu mimi yoyote, 625 show nilizopiga mwaka jana. mpaka sasa hivi kwa mwaka huu, nimefungua na koffi, nyuma nilikuwa na mikataba ya safari lager, sijui tigo, sijui nini, show zangu mwenyewe, show ni nyingi, 625 show nilizofanya mimi mwaka jana.kuna sengerema, magu,  wapi, mi huwa nahesabu tu show zangu, mikataba niliyofanya show 50 sijui 100 zote mi nafanya, hizo ni kazi zangu mie.nilikua na perform ijuma jumamosi na jumapili.."

"unajua sisi wasanii tunakula kilaini sana tuseme, tofauti na wafanyakazi wa serikalini anasubiri mshahara mwisho wa mwezi ushaelewa? hasa lazima nijitume kwasababu ni hela ambayo naipata kwa masaa mawili, kwa hiyo siwezi kusema najiskia uchovu sana siwezi kufanya kazi zingine huo ni unafki, kuna mtu anafanya kazi analipwa laki nne tu au laki mbili na anaenda kazini kila siku na anatumia nauli yake kwenda, mi nalipwa show milioni 2, milioni 3 nna wasiwasi gani, mwaka huu mpaka sasa hivi nina show 8, ndio nimeanza nina show 8." amesema H baba


NEYO: NIMESHAWAHI KUOA NIKIWA NA MIAKA 19

 Licha ya kujulikana kwa kufunguka na kuweka wazi mambo mengi ya kimapenzi katika nyimbo zake, nguli wa r&b Neyo ameweza kuficha siri yake kubwa kwa miaka mingi.


TMZ wameripoti kuwa Neyo amefunguka kuwa alishawahi kuoa akiwa na miaka 19, lakini ndoa yake haikudumu na ilivunjika kwa mda mchache baadae kwa kuwa alikuwa akipenda kuingia katika kazi ya muziki lakini mke wake alikua hataki kabisa na hakuwa akimpa sapoti.

"sasa hivi nipo hapa nilipo, na sijui yeye yuko wapi" alisema kwa utani.
kwa hivi sasa mshindi wa tuzo za Grammy, ameshaendelea na maisha yake ya kimapenzi na ana watoto wawili na girlfriend wake wa kitambo Monyetta Shaw

DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com